Tahadhari kabla ya hatari :)

Bado nacheka! Sana tena! Wajua, kuna huyu kaka alifikishwa mahakamani Jumatatu kwa sababu ya arafa hii:

“Ndizi alimuuliza chungwa, kwa nini ukiliwa lazima unyonywe? Chungwa akasema, mwenzio nisiponyonywa, sisikii raha kabisa, na wewe je? Ndizi akasema, mie nisipovuliwa nguo, sipati raha, passion (mkarakara) naye akadakia, mwenzenu mie nisipotiwa kidole halafu kizungushwezungushwe kwa ndani, sipati utamu kabisa, wewe je dada?”

Basi usimcheke. Ana utundu si haba, lakini, pana umalenga wa aina fulani katika arafa hii. Aliketi, akafikiria, akabuni, akaandika na kisha akamtumia msichana wa wenyewe.

Ole wake, hakujua kuwa sio kila mtu anafurahia uroda wa simu.

Alifikishwa kizimbani pap!

Sijui kama tumempoteza malenga, ama iwapo, badala yake ataandika tamthilia ya arafa. Ni wazo tu!

Comments

Popular posts from this blog

BOMAS LIVE---KENYA DECIDES--THE INSIDE STORY

Remembering Dr Margaret Ogola (June 12,1958 - September 21, 2011)

Four things Kenya’s ex-CJ Willy Mutunga told the BBC about Kenya’s politics