PART THREE: Babylon your days, are numbered!

Today is another day, to continue with my sheng' story I have been telling for the last three days. And Jeff 'Crucial' Mwangemi gets a hi-five for being such a nice guy.

Unajua ku-inspire ma-boy wa ghetto hadi ile style wanaona wako na Vision ndio kitu Jeff ame-do for a long time. Metro FM sikuhizi ndio inasikika kwa mat mob za Mathare, Kibera (Kibich), Ungwaro (kawangware) na hizo places zingine mob mob za wasee wanahandwa na makarao juu ya maisha msoto.

Yaani imagine, poverty ni crime, unakabwa, unasundwa ndani, ukitoka unaanza ku-hustle, unakutana na makarao one night, unarudi ndani “loitering” na “drunk and disorderly” ndio makosa. Ma-boy wa ghetto hukipitia.

Place nastay hapa Nairobi, wale wanajua Safari Park ni wapi na Zimmerman ni wapi, basi niko katikati. Kuna boy flani yeye hunishave nywele. Anaitwa Timo. M-nutty mbaya. Ana dready, yeye hu-smoke fegi, sijui kama yeye hu-smoke ndom pia, lakini haitakuwa surprise, coz conviction yake kwa doba ni fyam. Anaget message na anai-live.

Sasa kuna hii siku niko hapo na-shave. Msee hu-shave kichwa ama nywele…hehe. Anyway, hii day, kuna boy flani amezoea kupromise Timo kila day after amem-shave ati atamjenga. Lakini kila siku analipa tu ile finje.

So this time, Timo akamshow live: “Niaje wewe, kila siku unasema utanijenga, na unanitupisha mbao. Kwani umekuwa Vision 2030?”

“Usijali. Wewe ni boy wangu, nitakushughulikia major,” huyo msee akasema.

“Wacha. Promises are the comfort of a fool,” Tim akamshow. “Haina haja ushinde unasema uta… uta… uta…, kama ni kunicheki, act. Sio ku-promise, hiyo haiwezi work.”

Kumbuka huyu ni customer anaambiwa. Lakini ni beshte ya Timo, so manze commonsense kama hiyo na msee haoni, inakushow vile watu kama Timo, ni opportunity hawa-kuget. Lakini wako na ile roho ya kutaka ku-move kujijenga major. Ni wasee wako wise.

Kila day, anaamka asubuhi anafungua kinyozi. Hata kama maji hakuna, anakushow mapema vile hiyo siku hakuna massage na aftershave juu maji hakuna. So, mwenyewe unaamua kama utaendelea na shave ama uta-postpone.

Timo ni boy amenishow vitu mob. Experience zake za kushikwa akiwa kwa mabeshte Zimmerman (Zimmer) na kupelekwa ndani. Hadi anakushow vile police station gani ni poa.

“Food ya Kasarani ni poa. Nikikabwa, mii husikia tu nipelekwe huko, juu manze Lang’ata, Central na Kilimani ni stress,” alinishow day flani.

Ati ukishikwa, usiogope. Food ikiletwa, hata ukiona cockroach ndani, unamanga tu, juu hujui next time meal ita-come ni lini. Thank goodness, hiyo kushikwa yeye hulipa hizo ma-fine tu, soo tano, punch, na anatoka kurudi kuendelea na works.

Huyu ni kinyozi, unamwitisha punch na pengine hiyo ndio dough ame-make for a whole day. Surely, hii system ni ya majambazi. Ile kidogo uko nayo utanyang’anywa iongezewe wale wako nayo.

Na sio Timo pekee. Msee yeyote ashawahi panda mat za 44, anajua vile Roysambu ma-boy huwanga kibao. Ma-mechanic na ma-conductor wa mat, so sio surprise hao kuitwa Mungiki na ku-deadishwa. Si ati pengine Mungich hawako, zi. Lakini sio ati kila boy ni mungich, halafu I think dilemma ya makarao ni ku-identify msee kama mungich. So hao hushika ma-boy wote wanahang around hapo.

So asubuhi moja nikiishia job -- ma-six ndio ni-beat jam ya Thika Road, sonko asinimeze-- nilisikia conversation moja ikani-jolt conscience ile mbaya.

Ndio scandal ya Triton Petroleum ilikuwa imebreak.

Hii scandal, sh7.6 billion zilikuwa zimepotea kwa game flani ya mabudaa kuuza oil. Architect alikuwa mhindi flani anaitwa Yagnesh Devani na alikuwa ame-do hivyo aki-collabo na masonko kwa ministry ya Energy.

So, ika-happen, hii asubuhi, story ya Devani ilikuwa frontpage ya Nation. Na nilikuwa nimepiga collabo kwa hiyo story na colleague anaitwa David Mugonyi tuki-unravel Devani.

“Hebu cheki vile mabudaa wanatufinyilia chini. Hiyo chapaa yote inapotea halafu wanatushow ati hakuna job kwa gava (government),” boy mmoja alisema huku aki-flip flip paper akitingiza kichwa. Aka-click.

Wenzake wakaroll back hadi time Kiraitu Murungi, ule minister wa Energy at the time, alikuwa kwa scandal ya Angloleasing, “sahi ona kule ameishia. Halafu hakuna kitu atafanyiwa.”

Manze nilifeel huyu boy ile mbaya. Yaani sio choice yake kuwa konkodi. Kusoma anajua, ni opportunity hana ya kujiendeleza, na probably amezaliwa tao, mapero walidie na ocha hawana shake, so asipokuwa konkodi, crime ndio next ama ashinde ku-tarmac na kubembeleza mapanthree Kirinyaga na River Road wamsaidie. La sivyo, aishie akuwe hawker ama kazi ya mjengo.

Ndio, lazima watu wa-earn kutoka kwa jasho lao, lakini, ukicheki masonko wanareap place hawajasow any, inauma sana. Especially kama system ni kama hii ya majambazi, basi itakuwasha sana.

Ma-morning kwa hiyo Jam ya Thika road, hapo past Utalii, utacheki stream ya wasee kutoka Mathare wanatrek wakiishia job.

Wengine, utawapita along the way wamekaa down wanangojea lorry kutoka construction site i-come iwachukue waende mjengo. Ni kutafuta unga msee.
Unasikia risto za hawa wasee ati wanaamka ngware wafike mjengo angalau mapema ndio wachaguliwe foreman akiingia.

Wengine wameform tu-groups tudogo na wakabuy ma-spade na jembe, so officially hao ni wasee wa mjengo. Wasee wa mkono. Wanalink na foreman kwa site na kumshow vile watamsaidia works. Wananegotiate kama ki-group na ikiivana, wanajua hadi hiyo kazi iishe ndio wataanza kuhustle tena. Bora foreman asiwacheze. Kila day wa-earn bread yao, bas. Story inakatika. Lakini hii yangu tuonane ke-ke-ke-kesho!

Comments

Popular posts from this blog

The Cockroach Dance

BOMAS LIVE---KENYA DECIDES--THE INSIDE STORY

Remembering Dr Margaret Ogola (June 12,1958 - September 21, 2011)